Recent Posts

SUNDEY OLISEH KUWA KOCHA NIGERIA



Imebaini kuwa kiungo  wa kati wa zamani wa Super Eagles ya Nigeria, Sunday Oliseh anafanya mazungumzo na shirikisho la soka la Nigeria NFF kwa nia ya kutangazwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria.

Oliseh ambaye alikuwa nahodha  wa zamani wa Super Eagles mwenye umri wa miaka 40 aliingoza timu hiyo katika mechi 63 za kimataifa.


Kwa mujibu wa mwandani wetu Oliseh anatarajiwa kutangazwa karibuni kuwa kocha mpya.
NFF ililazimika kufanya bidii ilikuziba pengo lililoachwa wazi na Stephen Keshi aliyefutwa kazi mwishoni mwa juma.

Oliseh alikuwa miongoni mwa kikosi cha taifa kilichotwaa kombe la mataifa ya Afrika mwaka wa 1994 na kisha nishani ya dhahabu ya olimpiki mwaka wa 1996 .

Oliseh vilevile alikuwa katika kikosi kilichoiwakilisha Nigeria katika kombe la dunia la mwaka wa 1994 na 1998.

Super eagles ilifuzu katika mkumbo wa 16 bora katika mashindano hayo mawili na Oliseh anakumbukwa kwa bao lililoisaidia Nigeria kuibana Uhispania katika mechi za makundi.

Kizazi chake kinatajwa na wengi kuwa maarufu zaidi katika historia ya soka ya nchi hiyo kwa pamoja na Jay-Jay Okocha, Nwankwo Kanu na Finidi George.

Oliseh amekuwa akihudumu kama mtangazaji wa kandanda mbali na kuwa mshauri wa FIFA wa maswala ya kiufundi.

Japokuwa Oliseh hana khariba ya kufunza timu ya taifa aliwahi kuifunza timu ya daraja la pili la Ubeljiji Vervietois kati ya mwaka wa 2008 na 2009.

Iwapo atatangazwa kuwa kocha wa Nigeria Oliseh atachukua hatamu kutoka kwa mkurugenzi wa kiufundi wa NFF Shaibu Amodu na kocha msaidizi Salisu Yusuf.

SUNDEY OLISEH KUWA KOCHA NIGERIA SUNDEY OLISEH KUWA KOCHA NIGERIA Reviewed by Unknown on 13:06 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.