Baada ya kujitokeza na kuweka nia ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya CCm Viti maalum mkoani Singida nyota wa filamu Nchini Tanzania, Wema Sepetu ameshindwa kutimiza Ndoto hiyo kwa mwaka huu 2015 baada ya kushindwa katika kura za maoni.
Wema Sepetu alijipatia kura 90 huku Aysharose Mattembe akiongoza na kura 311 akifuatiwa na Martha Mlata mwenye kura 235
na Diana Chilolo mwenye kura 182.
Hatua hii inakuja kufuatia kuwepo kwa upinzani mkali dhidi ya wagombea wengine walio kuwepo katika kinyanganyiro hicho cha ubunge hivyo kupelekea Wema kukosa dhamana ya kuwawakilisha kwenye viti
maalum vya ubunge.
Kupitia Instagram Wema aliandika maneno haya.. "Nilivyoamua kugombea viti maalum, nilijua kuna
kupata na kukosa. Awamu hii nimekosa, ila dunia bado inazunguka nawapongeza walioshinda. Nawashukuru
mlioniunga mkono, Mungu aendelee kuwabariki kwa mapenzi yenu juu yangu, yananipa moyo nawashukuru pia wote mlionipinga maana mmeniongezea ujasiri na nina nguvu mpya ya kuthubutu upya 2015 ni mwaka wa kipekee kwenye muamko wa
vijana Tanzania. Bigger things loading.. Most of
all Nilizaliwa nikiwa katika Chama Cha Mapinduzi
na nitakufa nikiwa ndani ya Chama Cha
Mapinduzi…. Safari yangu ya Siasa ndo kwanza
inaanza.”
No comments: