Dokta John Pombe Magufuli,amekuwa akitajwa kila kona ya Tanzania kwamba ndie atakaekalia kiti cha Ikulu ya Tanzania.
Magufuli ambae alikuwa waziri wa ujenzi,amepewa matumaini makubwa,baada ya kutinga mpaka tatu bora huku akifukuziwa na wamama wawili,Amina na Dokta Asha Rose Migilo.
Japokuwa mchuano ni mkali,ila kila mmoja akipewa nafasi kwa uwezo wake wa kuliongoza taifa kikamilifu bila ya matatizo yeyote ile.
Hata hivyo watanzania wengi wameonekana kumkubali maguli kwa kuwa ni waziri aliyefanikisha mambo mengi katika wizara yake na kutatua matatizo ya usafiri barabarani.
ISambamba na hayo macho na masikio ya Watanzania wanasikilizia na kusubilia hii leo nani atatangazwa kuwania uraisi wa Tanzania,ambapo mpaka sasa mchakato unaendelea katika ukumbi wa chama cha mapinduzi CCM mkoani Dodoma.
No comments: