Klabu ya Liverpool nchini Uingereza
imefanikiwa kumsajiri mshambuliaji wa Klabu ya Aston Villa Christian Benteke kwa kitita cha pauni milioni 32.5.
Liverpool imekubali kutoa kitita hicho baada ya kupokea kitita cha pauni milioni 49 kutokana na mauzo ya mchezaji Raheem Sterling aliyehamia Mancity.
Benteke aliyekuwa amesalia na kandarasi ya miaka 2 katika klabu ya Villa anaungana na wachezaji waliosajiliwa na Liverpool msimu huu ili kukiongezea nguvu kikosi cha Brendan Rodgers.
Ukiachana na Benteke wachezaji waliosajiliwa na Liverpool mpaka sasa ni Dan Ings, Divok Orig aliyekuwa kwa mkopo lile, James Milner, Joe Gomez, Roberto Filminho, Bogan, Natahiel Clyine
Benteke anatarajiwa kuziba pengo la Mshambuliaji wa Uingereza aliyemajeruhi Daniel Sturridge, Sturridgealiichezea timu hiyo mara 18 msimu uliopita kutokana na msururu wa majeraha na atasalia nje hadi mwezi Septemba akiuguza jeraha la kiuno.
BENTEKE ATUA RASMI LIVERPOOL
Reviewed by Unknown
on
15:30
Rating:
No comments: