Mwanzilishi na Mmiliki wa Cash Money records, Birdman 'Baby' ambaye pia anasimama kama Baba mlezi wa rappa Lil-Wayne amefunguka juu ya madai ya Weezy kutaka kujitoakatika kundi la Young Money wala kutotoa mchango wowote kwa upande wa Cash-Money kwa madai kuwa kitendo cha bossi wao ambaye ni Birdman mwenyewe kukataa kutoa Albamu yake ya The Carter V ni unyonyaji na asingependa kujihusisha nao tena katika uzalishaji wa kazi zake licha ya kudai si rahisi kujitoa kama inavyo dhaniwa.
Birdman 45 amesema hakuna nafasi ya kuondoka kwa Lil Wayne kwenye record lebel ya Young Money ambapo amedai kuwa ataenda mahakamani kuweka kizuizi cha Weezy kujitoa katika kundi hilo.
Kupitia MTV_NEWS taarifa zinasema kuwa maamuzi hayo ya Birdman yamekuja kufuatia kuchukizwa
na maneno aliyo andika Lil Wayne kwenye acount yake ya twitter kuwa
Kitendo cha albamu yake ya Carter V kuzuia ni utumwa na unyonyaji pia
Licha ya mikataba waliyo nayo
Young Money pamoja na Cash-Money.
Fahamu kitendo cha Birdman kufanya maamuzi hayo ikiwa ni pamoja na kutaka kwenda mahakamani kumzuia Lil-Wayne kujitoa ni baada pia ya tetesi kumfikia kuwa yeye ni mnyonyaji wa nguvu kazi za marappa wa Young-Money.
Pia fahamu kuwa album ya Lil-Wayne ya The Carter V itatoka mpaka Birdman atakapoamua itoke licha ya kudai kuwa yeye huzingatia biashara kwanza na muda ingawa kauli zimepishana na Lil-Wayne anayetaka itoke kwa wakati huu.
No comments: