Kupitia Single ya Nicki Minaj ya ’Only’ wiki iliyopita imemuwezesha kushika nafasi ya kwanza kwenye Hot R&B/Hip-Hop Songs
chart za Billboard, na kumfanya awe msanii wa kike
aliyewahi kuwa na nyimbo nyingi zaidi zilizofika
nafasi ya kwanza tokea chati hizo zianzishwe
miaka 56 iliyopita ambapo pia rekodi hiyo ilishawahi kushikiliwa na
Missy Elliot aliyekuwa na nyimbo tatu zilizokamata
nafasi ya kwanza kwenye Billboard, huku Minaj
sasa akiwa amefikisha nyimbo nne.
Tukio hilo limeambatana na kumletea wiki ambayo rappa huyo wa kundi la Young Money ameonekana
kwenye vituo vya tv na kusikika kwenye radio,
ambapo pia amepata bahatii ya kuonekana kwenye majarida makubwa na
interview za vituo vingi vya Redio na Tv na yote haya yakiwa ni fursa kamili ya kutangaza album yake mpya Pink Print.
Wiki iliyopita Nicki Minaj amechaguliwa kuwa sura mpya
ya Mbunifu wa mavazi Roberto Cavalli, ikiwa ni pamoja na kupiga picha za Fashion mpya kutoka kwa mbunifu huyo wa mavazi.
Fahamu pia wiki iliyopita pia Minaj wakati akizungumzia nyimbo
aliyofanya na Beyonce ‘Flawless Remix’ aliweza kugusia namna ambavyo Jay Z, mume wake
Beyonce ameikubali sana kazi hio kitu ambacho
kimempa moyo sana kuzidi kuipenda kazi yake ya Muziki na kudai kuwa yeye ndio rappa bora wa Kike Duniani.
No comments: