Raia wa Ufaransa, Jacques Sayagh ambaye ni mtunisha misuli (Body Builder), amebuni njia ya kurahisisha maisha yake kwa kuishi mitaani kwa madai kuwa nyumba isingemtosha wala kumpendeza kwa shughuli zake za Utunishaji Misuli na kudai kitendo cha yeye kuishi mitaani na kulala chini ni bora kutokana na kazi anayoifanya na kudai kuwa anapoamkia ndipo hufanyia Mazoezi yake.
Jacques Sayagh 50, amekua akizagaa mitaa mbali mbali katika jiji la Paris, Ufaransa na kulala katika mitaa hiyo ambapo kila ifikapo asubuhi alipoamkia ndio hufanyia mazoezi kutokana pia na kutembea na Vifaa vyake kitu ambacho kimeushangaza umati mkubwa wa watu katika jiji la Paris.
"Sitaki kuishi kwenye Nyumba hali ni ndogo na watu hawaelewi sababu ya mimi kulala sakafuni, lakini huwa hata sisikii baridi na ndio Maisha ninayo ya penda", alisema Sayagh.
Jacques pia amedai licha ya kuwepo kwa majira ya baridi kali katika jiji la Paris, lakini huwa haimzuii kulala mitaani na kufanya shughuli zake za Utunishaji Misuli.
"Watunisha misuli tumejaliwa kuishi kokote na tunaweza thubutu kufanya jambo lolote", alisema Jacques ambaye pia alidai kushinda mashindano mbali mbali ya Utunishaji misuli licha ya kuathirika na unywaji pombe kupita kiasi.
"Nina wajukuu ilasitaki wafikirie kuwa babu yao ni Mshenzi, ninachotaka tu wajivunie kuwa na Babu kama mimi!, ni hicho tu!" alisema Sayagh wakati akihojiwa na mwandishi wa habari Julien kupitia makala inayomuhusu itwayo 'SAYAGH's DAILY WORKOUT ROUTINE.
No comments: