Watu wapatao 20 wameuawa na wengine kadhaa
wamejeruhiwa kutokana na mapigano ya makabila
yaliyotokea huko Jamhuri ya Afrika ya kati.
Taarifa kutoka Jamhuri ya kati zinasema kuwa
ghasia hizo zilizuka tangu ijumaa ya wiki iliyopita na
kuendelea ambapo raia wengi walipigana,na wengi
wao walikuwa kundi la Antibalaka ambao ni wakristo.
Hata hivyo taarifa kutoka vyombo mbali mbali vya
habari zinasema kuwa Wapiganaji hao wa kundi la
Antibalaka walianzisha mashambulizi dhidi ya kundi
la wapiganaji wa waasi la Seleke,na mapigano hayo
yalitokea katika mji mkuu wa Bangai, ambapo katika
mji huo wapiganaji wa kundi la Seleke walionekana
wakirandaranda na magari yao pembeni mwa mji huo
Bangui.
HALI BADO TETE JAMHURI YA KATI:
MAPIGANO MAPYA YAZUKA TENA
Reviewed by Unknown
on
10:07
Rating:
No comments: