Recent Posts

PUFF DADY 'DIDDY' AMPIGA DRAKE NDANI YA CLUB

Katika tukio ambalo linaweza kuzua visasi kwa mashabiki wa damu damu, wa Drake na Diddy ni hili la Diddy kumpiga ngumi Drake usiku wa jumapili katika Club ya LIV iliyopo Miami marekani katika usiku wa birthday ya Dj-khaled.

Kwa mujibu wa MTV News imeelezwa kuwa aliye anzisha ugomvi ni Puff-Dady mwenyewe akimshutumu Drake kuperform nyimbo yao walioshirikiana japo haijajulikana,bila ya kutimiza idhini kamili na kibali kutoka kwake, ambapo taarifa zaidi zimeleza kuwa baada ya maneno makali aliyopokea Drake kutoka kwa Diddy ndipo ngumi ilifuata na kumpata Drake kufuatia hasira alizokuwanazo Diddy ambapo Drake alianguka chini na shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni Dj wa rappa Rick Ross anayeitwa Dj Sam Sneaker alitoa maelezo kamili kupitia acount yake ya Twitter juu ya tukio hilo.

Sam Sneaker aliandika kuwa Diddy alirusha ngumi ambayo haikumkosa Drake na kumfanya aanguke chini, hata hivyo mashuhuda wengine pia walieleza kuwa baada ya kupigwa ngumi Drake alielekea Hospitali kufuatia maumivu ya bega aliyoyapata baada ya kuanguka chini japo haikuelezwa ni Hospitali gani alielekea na aliumia kiasi gani.

Alicho kiandika Twitter Dj Sam Sneaker baada ya kushuhudia tukio hilo ni hiki hapa:
"Diddy put hands on that boy...and he ain't go 0-100
that boy left
Yall pray for Drake, it definitely wasn't bout Cassie
-Sam Sneak @Djsamsneaker

Hata hivyo kuna madai ya wawili hao kutopatana kwa muda licha ya kupatanishwa mwaka jana katika tamasha la OVO Festival lililofanyika Toronto ambapo Drake alipo hojiwa alisema kuwa ni "Falme mbili tofauti" kati yake na Diddy.

Madai mengine ya chanzo cha ugomvi huo huenda ikawa pia mpenzi wa Diddy, Cassie kufuatia mtindo wa Drake wa Uplay boy wa kuchukua wapenzi wa wenzie kama alivyofanya kwa Chris Brown kutoka na Rihanna na hivi karibuni kudaiwa kutoka na Karrueche huku baadhi ya watu wakidai kitendo hicho huenda kikawa furaha ya kisasi kwa Chris Brown baada ya kukosa nafasi kama hiyo ya kumpiga ngumi Drake.

PUFF DADY 'DIDDY' AMPIGA DRAKE NDANI YA CLUB PUFF DADY 'DIDDY' AMPIGA DRAKE NDANI YA CLUB Reviewed by Unknown on 22:06 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.