Recent Posts

IMANI ZA KISHIRIKINA ZAMPELEKEA MAMA KUTAKA KUMTUPA MWANAE KATIKA KISIMA CHA MAJI.

Kutokana na vitendo vya kishirikina kukithiri Nchini Tanzania, mwanamke mmoja amekutwa akitaka
kumtumbukiza mwanaye wa kiume  anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka mitano hadi saba kwenye
kisima cha maji, kutokana na kinacho dhaniwa
kuwa ni imani za kishirikina, katika eneo la Kihonda
Mkoani Morogoro.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Veronica Madebe amezua hali ya sintofahamu katika mtaa wa
Azimio, kata ya Kihonda katika manispaa ya
Morogoro, baada ya kukutwa akitaka
kumtumbukiza mwanaye wa kiume  ambaye ni
pacha, mwenye umri wa kati ya miaka mitano
hadi saba kwenye kisima cha maji, kutokana na
kinachosadikiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Tukio hilo limejiri jana katika eneo la Azimio,
baada ya mwanamke huyo kukutwa na mmiliki
wa nyumba kilipo kisima hicho, aliyejulikana kwa jina la Dani Haji,
akijaribu kumtumbukiza kisimani mmoja wa
watoto wake pacha, kwa madai  yaliyoelezwa
huenda ni kupungukiwa akili, ama ni imani za
kishirikina.

Veronica alidai kufanya kwake hivyo kumetokana nakutumwa na wakazi wawili wa eneo
hilo kufanya hivyo, na wakati mwingine kudai
alikuwa kwenye kifungo na alipaswa kutoa
kafara ya mtoto wake kwa kumtupa kisimani ili
afunguke baada ya kuokoka kiimani, jambo
lililothibitishwa pia na mmoja wa wajumbe wa
serikali za mitaa katika eneo hilo
Mmoja wa familia iliyotajwa na mwanamke
huyo kufanya kitendo hicho cha kikatili,
kilichozuiwa na wasamaria wema, ambapo alikiri
kumfahamu mwanamke huyo lakini bila kuwa
na matatizo yeyote, na alishangazwa na hatua
hiyo na alipomuona aliamua kumvaa yeye na
mtoto aliyekuwa amembeba, bila sababu zozote,
hadi alipoamuliwa na kundi la wananchi
waliojitokeza.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Wananchi wa eneo hilo walipigasimu polisi
kuomba msaada wa dharura na kumpeleka
mama huyo katika ofisi za mtendaji wa kata ya
Kihonda, ambako ulinzi mkali wa polisi
uliimarishwa, na baada ya muda mwanamke
huyo alitolewa na kuingizwa kwenye gari ndogo
kwa nia ya kupelekwa polisi, lakini ilidaiwa kuwa kitendo cha mwanamke huyo kilisababisha vurugu hadi polisi walipoingilia kati na
kumpakiza kwenye gari na kuondoka naye.

IMANI ZA KISHIRIKINA ZAMPELEKEA MAMA KUTAKA KUMTUPA MWANAE KATIKA KISIMA CHA MAJI. IMANI ZA KISHIRIKINA ZAMPELEKEA MAMA KUTAKA KUMTUPA MWANAE KATIKA KISIMA CHA MAJI. Reviewed by Unknown on 22:51 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.