Ilikua ni siku moja tu ambayo kama ingekua Israel na
Parestina basi kungekuwa na umwagaji damu kati ya
Tanzania na Nigeria kwa upande wa mashabiki wa
Davido na Diamond ambapo msanii Davido aliukera
wingi wa umati wa Watanzania waliokuwa online
kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii nchini
Tanzania Jumapili hii iliyoisha.
Tukio hilo lilitokea wakati mwakilishi kutoka Tanzania
katika shindano la Big Brother Africa, Idris Sultan
kutangazwa mshindi wa Big
Brother Africa, huku wakati huo huo Davido alitweet
post ambayo ilizua utata iliyokuwa imeandikwa hivi:
“N they cheat again lol,”.
Dakika chache baada ya staa huyo wa Nigeria
kuandika hivyo, watumiaji wengine wa mitandao ya
kijamii walianza kumshambulia kwa matusi staa huyo
huku Wengi
wakiicapture tweet hiyo na kuipost kwenye
Instagram pamoja na Facebook na kumuandama
vikali hata kuthubutu kumtusi Mama yake Mzazi.
KWA NINI DIAMOND AMKOSEA DAVIDO??!!
Kama ilivyo ada ya KAY STALLION ENTERTAINMENT ni kukupa
habari zenye uhakika kutoka vyombo mbali mbali vya
habari, na sehemu mbali mbali sasa basi hiki ndicho
kilichopelekea Platnumz kuonekana kumkosea
Davido ambapo baada ya kuchukua tuzo nyingine
Nchini Nigeria katika tuzo za Future_Awards_Africa
zilizo fanyika Lagos, Nigeria usiku ambao Idris
alishinda BBA ambapo Diamond aliweka picha
Instagram ya tuzo hiyo ikiwa na meneja wake huku
maneno aliyo ya weka kupelekea watu kujua yakuwa
alicho kiandika Davido lilikuwa jungu kwa Watanzania
ambapo Diamond aliandika hivi:
"Thanks God we have cheated another one on The
Future Awards Africa in Lagos Nigeria # Same Day
#Same Night" huku ikilinganishwa na ya Davido
katika Twitter ya "N they cheat again lol" na kugeuka
njia ya Davido kupokea matusi na kejeli nzito kutoka
kwa Watanzania.
Fahamu kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forum
na maoni mbali mbali ya wadau ambapo
imefafanuliwa na Mwanachama mmoja wa mtandao
huo kwa kuandika hivi:
Status ya Davido aliyoandka ''N they cheat again lol!''
imetafsiriwa vibaya na watanzania
na kuonesha kipaji chao cha matusi
WAKAMTUSI MAMA YAKE.
Diamond ndie mtu wa kwanza anatakiwa
kulaumiwa kwani alikurupuka baada ya
kuandika ''Yeah we cheat again same night''
Yeye ndiye aliyewafanya watu wamshambulie
DAVIDO kuwa alimaanisha sisi tumecheat
kupata tuzo.
UKWELI NI HUU, Davido aliandka vile juu ya
tukio la CRIS BROWN NA mpenzi wake
KARUUCHE ambao walidanganya duniani
wameachana na kusameheana.
DAVIDO aliona kama drama! akaona
wametudanganya tena kwani si mara ya
kwanza kutengana kama wana bifu na
kurudiana.
Ukifuatilia twiter utaona BROWN na
KARUUCHE wakitukanana juu ya ishu ya
DRAKE huku still wanapendana na bado
wapenzi.
PILI sisi hatutoi tuzo wala hatupangi big
brother kama Davido mnasema aliongelea juu
ya ushindi wa big brother basi haiwahusu
ninyi inawahusu big brother ambao ndio
wanaendesha mchakato wa mshndi.
NDIO MAANA KASEMA THEY CHEAT AGAIN
wao BBA si nyie Nigeria wamekosa ushindi
karibu miaka 5 mfululzo.DIAMOND JIFUNZE
MAISHA NI WATU.
Credits_to_Jamii_Forum .
No comments: