Recent Posts

JIBU KAMILI LA UTATA WA KUZALIWA PENZI JIPYA KATI YA CHRIS BROWN NA AMBER ROSE BAADA YA KUFUMWA KLABU WAKICHEZA KAMA WAPENZI.

Baada ya kuzaliwa tetesi ambazo kwa haraka haraka mtu yeyote asingeweza kubisha kuwa Amber Rose na Chris Brown ni wapenzi wapya kufuatia wawili kukutwa Club wakicheza kimahaba kama NEW CUPLE huku kila mmoja akiwa ameachwa na mpenzi wake nyakati za hivi karibuni.

Unaambiwa Amber Rose pamoja na Black Chyna ambaye ni mama wa mtoto wa Tyga walikutana na Chris
brown kwenye club moja maarufu huko LosAngels Marekani, ambapo waliweza kujiachia usiku kucha na kupelekea marafiki na watu wa karibu  na Chris Brown kuona kama ni tukio la ajabu na huenda kwa akili ya Chris akasubutu kumtongoza au hata kuenda kulala naye kama mpenzi na huenda asinge weza kueleweka kwa washkaji zake, Tyga na Wiz Khalifa ambao wasinge stahimili maneno ya Media mbali mbali juu ya tukio kama hilo endapo lingetokea lakini kumbe ilikuwa kwa ajili ya burudani tu na kuondoa Stress za kuachwa na wapenzi wao katika nyakati zilizo pishana.

Hata hivyo kuna baadhi ya watu walidai kuwa Chris alikuwa anamfukuzia Amber kimya kimya ila hakupata nafasi na hivyo kuanza kutumia misemo isiyo eleweka kupitia mitandao ya kijamii hususani Instagram na Twitter ambapo moja ya ujumbe wa utata ulio hisiwa kuwa huenda ilikuwa njia ya Chris kujivuta kwa Amber ni huu alio post Instagram uliosema hivi:

Boyfriend: Roses or daisies?
Girlfriend: Daisies
Boyfriend: Okay just wondering what
I should put on your casket after I
murder that p***y

Hata hivyo taarifa zaidi kutoka vyombo mbali mbali Marekani zimedai kuwa hakuna jipya kati yao na ilikuwa njia tu ya wao kuonyesha kuwa hata furaha hupatikana pia katika Single life na sio Engaged au Married.

JIBU KAMILI LA UTATA WA KUZALIWA PENZI JIPYA KATI YA CHRIS BROWN NA AMBER ROSE BAADA YA KUFUMWA KLABU WAKICHEZA KAMA WAPENZI. JIBU KAMILI LA UTATA WA KUZALIWA PENZI JIPYA KATI YA CHRIS BROWN NA AMBER ROSE BAADA YA KUFUMWA KLABU WAKICHEZA KAMA WAPENZI. Reviewed by Unknown on 05:37 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.