Recent Posts

MAMBO MUHIMU UNAYO PASWA KUYAJUA KUHUSU THIERY HENRY MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA ARSENAL ALIYESTAAFU SOKA JUZI

>>Baada ya Mshambuliaji wa zamani ya timu ya Taifa ya Ufaransa na Klabu ya Arsenal Thierry  Henry kutangaza rasmi kustaafu soka akiwa na klabu ya New York Red Bulls inayoshiriki ligi kuu ya Marekani maarufu kama Major League Soccer, K-STALLION inakuletea historia yake kwa ufupi ili upate kumfahamu kwa undani.

Jina lake kamili anaitwa Thierry Daniel Henry alizaliwa August 17  mwaka 1977  katika mji wa  Les Ulis, Essonne kitongoji kilichopo Paris nchini Ufaransa toka akiwa mdogo alitajwa kama atakuja kuwa mshambuliaji bora .

Alisajiliwa na AS Monaco mwaka 1990 na  alianza kucheza soka la kulipwa mwaka 1994 akiwa na miaka 17. Kwa mara ya kwanza aliitwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa mwaka 1998, Wakati akiichezea Juventus ya Italy ambao walikuwa  mabingwa wa wakati huo

Akiwa Juventus  Henry alikuwa akicheza  nafasi ya Winga mshambuliaji lakini hakuwa na msimu mzuri ndipo akajiunga na klabu ya Arsenal kwa ada ya paun milioni 11 mwaka 1999 ambapo kocha Arsene Wenger alimbadilisha namba na kumchezesha kama mshambuliaji wa mwisho.

Baada ya hapo Hery alianza kupata umaarufu mkubwa  akiwa na Arsenal kiasi cha kutajwa kuwa ni mmoja wa washambuliaji  mahiri waliowahi kutikisa kwenye ulimwengu wa soka, Japo mwanzoni alipata shida kwenye Premier League.

Chini ya kocha Arsène Wenger, Henry alifunga magoli 228 kwenye michuano yote na kuwa mshambuliaji mwenye mabao mengi kwenye historia ya washika bunduki wa jiji la London pia
kuwa mmoja ya washambuliaji bora wa wakati wote wa klabu ya Arsenal.

Kwa upande wa mataji Henry akiwa Arsenal alitwaa mataji mawili ya ligi kuu ya England, mataji matatu ya FA, pia  aliwahi kushika nafasi ya pili mara mbili kwenye tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA.

Henry amewahi kutwaa tuzo mbili ya mchezaji bora wa mwaka nchini England, pia mchezaji bora wa mwaka anayechaguliwa na wachezaji wenzie mara tatu.
Miaka miwili ya mwisho ya Henry akiwa Arsenal alikuwa nahodha wa  timu hiyo na aliiongoza Arsena kucheza fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2006 kwa mara ya kwanza katika historia ya Klabu.

Aliichezea Arsenal kwa miaka 8 na June mwaka 2007  Henry alijiunga na Klabu ya FC Barcelona kwa ada ya paun milioni 24. Mwaka 2009  alikuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kilichotwaa mataji matatu La Liga, Copa del Rey pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Aidha akiwa na Barcelona alifanikiwa kutwaa taji la Supercopa de España,  UEFA Super Cup na FIFA Club World Cup, pia Henry alitajwa kwenye kikosi cha timu bora ya mwaka  mara tano.

Mwaka 2010  alijiunga na klabu ya New York Red Bulls inayoshiriki ligi kuu ya nchini Marekani maarufu kama Major League Soccer na  kufanikiwa kutwaa taji la Eastern Conference mwaka 2010.

Alirejea Arsenal kwa mkopo wa miezi miwili mwaka 2012. Pia Mwaka 2013 Henry akiwa na New York Red Bulls alitwaa tuzo ya mashabiki wa MLS ijulikanayo kwa jina la ngao.

Kwa upande wa timu ya Taifa Henry aliwahi kupata mafanikio akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa,  alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 1998, pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa taji la UEFA Euro mwaka 2000 na taji la kombe la mabara mwaka 2003 ambapo alifunga bao la ushindi dhidi ya Cameroon.

October mwaka 2007 Henry alivunja rekodi ya gwiji wa zamani  Michel Platini kwenye timu ya taifa ya Ufaransa kwa  kuwa mfungaji wa wakati wote timu ya taifa hilo.

Henry alistaafu soka la kimataifa mwaka 2010 baada ya fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini ambapo timu yake ilitolewa katika hatua ya makundi. Na sasa amejiunga na Kituo cha Uchambuzi wa Masuala ya Soka Super Sport.

Nje ya uwanja, Henry ni msemaji wa masuala ya ubaguzi wa rangi kwenye mpira wa miguu hiyo inatoka na kuwa muhanga wa matukio ya namna hiyo. Alimuowa mwanamitindo wa England Nicole Merry mwaka 2003 na wana mtoto mmoja wa kike, ingawa wawili hao walipeana talaka mwaka 2007.

Huyo ndio  Thierry Daniel Henry au waweza muita CHAI  JABA.

By Sports Admin Emmanuel Senny
Source: Wikpedia

MAMBO MUHIMU UNAYO PASWA KUYAJUA KUHUSU THIERY HENRY MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA ARSENAL ALIYESTAAFU SOKA JUZI MAMBO MUHIMU UNAYO PASWA KUYAJUA KUHUSU THIERY HENRY MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA ARSENAL ALIYESTAAFU SOKA JUZI
Reviewed by Unknown on 13:34 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.