Recent Posts

MADRID YATWAA UBINGWA WA DUNIA UPANDE WA VILABU KWA MARA YA KWANZA

>>Mabingwa wa Ulaya msimu wa 2013-2014 Real Madrid wameendeleza ubabe wao wa kunyakua vikombe baada ya kutwaa Taji la Ubingwa wa Dunia kwa Vilabu baada ya kuwafunga mabingwa wa bala la Amerika ya Kusini timu ya San Lorenzo mabao 2-0.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Marraksh nchini Morocco, Madrid ilijipatia bao lake la kwanza kupitia kwa Sergio Ramosi mnamo dakika ya 37 na bao la pili lilifungwa na Gareth Bale dakika ya 51.

Madrid imeendelee kujiongezea makombe baada ya  mwaka jana kuchukua ubingwa wa Ulaya, Copa De Ray, Spanish Super Cup, Uefa Super Cup na sasa Club World Cup.

Kwa ushindi huo Madrid imeendelea kuweka rekodi ya kutokupoteza mchezo hata mmoja baada ya kushinda michezo 22 mfululizo katika mashindano yote.
Real Madrid: Casillas, Carvajal (Arbeloa 73), Pepe, Sergio Ramos (Varane 89), Marcelo (Fabio Coentrao 44), Ronaldo, Kroos, Rodriguez, Bale, Isco, Benzema.
Akiba: Navas, Khedira, Hernandez, Nacho, Jese, Illarramendi, Medran, Pacheco.
San Lorenzo: Torrico, Yepes (Cetto 61), Mas, Kannemann, Mercier, Buffarini, Kalinski, Barrientos, Ortigoza, Cauteruccio Rodriguez (Matos 68), Veron (Romagnoli 57).
Akiba: Franco, Arias, Villalba, Blandi, Cavallaro, Catalan, Fontanini, Quignon, Devecchi.

Picha zaidi: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2882085/Real-Madrid-2-0-San-Lorenzo-Sergio-Ramos-Gareth-Bale-score-European-champions-win-Club-World-Cup.html#ixzz3MYcYIGiP

MADRID YATWAA UBINGWA WA DUNIA UPANDE WA VILABU KWA MARA YA KWANZA MADRID YATWAA UBINGWA WA DUNIA UPANDE WA VILABU KWA MARA YA KWANZA Reviewed by Unknown on 10:45 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.