>>Mpambano wa watani wa jadi wa Ligi ya England uliokuwa ukisubiliwa na wengi na ukichukuliwa kama wa kisasi umemalizika kwa Mashetani wekundu Man Utd kujivua uteja kwa wachovu Liverpool baada ya mwaka jana Man U kupoteza mechi zote walizokutana na Wachovu wa sasa Liverpool.
Man U imefanikiwa kuibuka na ushindi mnene wa mabao 3-0 huku ikionekana kuwa na nafasi ya kupata mengine kama mchezo ungeendelea.
Wayne Ronney alikuwa wakwanza kuipatia bao Man katika dk ya 12, wakati bao la pili lilifungwa na Mhispain Juan Mata dk ya 40 na Robin Van Pers akahitimisha karamu ya mabao kwa bao lae la dk ya 71 lililotimiza idadi ya mabao 3 huku Liverpool wakiambulia patupu.
Kwa ushindi huo Man imefikisha point 31 na kukwea hadi nafasi ya 3 ya msimamo wa Ligi ikiachwa pointi 8 na vinara Chelsea yenye point 39 kileleni wakati Man city ikishika nafasi ya Pili na Pointi 36.
No comments: