>>Baada ya kushuhudia droo ya Ligi ya Mabingwa
barani Ulaya hatua ya 16 bora, Nayo Ligi ndogo ya
UEFA maarufu kama UEFA Europa League nayo
imetangaza ratiba yake ya hatua ya 32 bora ikihusisha
timu 24 zilizofuzu hatua ya makundi na zingine 8
zimeungana na timu hizo kutoka Ligi ya Mabingwa
baada ya kushika nafasi ya tatu katika makundi yao na
kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora hivyo
zimejumlishwa katika UEFA Europa League na
kutimiza idadi ya timu 32.
Liverpool ni moja ya timu zilizoshindwa kufudhu hatua
ya 16 bora katika Ligi ya Mabingwa baada ya kushika
nafasi ya tatu katika kundi lake hivyo kuungana na
timu za AS Roma, Ajax, Besikitas, Olympiacos, Athletic
Bilbao, Zenit, Fiorentina kushiriki Ligi hiyo ndogo
baaada ya kushindwa kwenye aligi kubwa.
Ratiba kamili ya UEFA Europa League hatua ya 32 bora
iko kama ifuatavyo;-
Young Boys vs Everton
Torino vs Athletic Bilbao
Sevilla vs Borussia Monchengladbach
Wolfsburg vs Sporting Lisbon
Ajax vs Legia Warsaw
Aalborg vs Club Brugge
Anderlecht vs Dinamo Moscow
Dnipro vs Olympiacos
Trabzonspor vs Napoli
Guingamp vs Dynamo Kiev
Villarreal vs Salzburg
Roma vs Feyenoord
PSV vs Zenit
Liverpool vs Besiktas
Tottenham vs Fiorentina
Celtic vs Inter.
Michezo hiyo itapigwa Februari 19 mwaka 2015 kwa
michezo ya nyumbani na ugenini ili kupata timu
zitakazofudhu hatua ya 16 bora.
No comments: