Recent Posts

ZIJUE 'BEEF' NANE ZA KIJINGA ZILIZO DUMU KWA MIAKA KADHAA HUKU ASILIMIA KUBWA ZIKIWAA ZA 2014 ZA WASANII WA HIP-HOP

Licha ya kuwepo mikwaruzano ambayo ilipelekea watu kuamini mwisho wa siku mambo yangeweza kuwa kama ya B.I.G na 2PAC baada ya kuonekana kuna wasanii wangeuana kamasio kutengeneza pande ambazo zingechukiana kupita maelezo lakini wachambuzi wa mambo wanakuambia katika beef zilizo tokea mwaka huu na kuonekana za kijinga ni hizi hapa:

Kuna baadhi ya marappa beef zao zimeonekaba kuwa ni njia ya kutafuta 'Kick' kwenye vyombo vya habari na kugeuka kuwa njia rahisi ya kuinua kazi zao, moja kwa moja tukianza na 50 Cent ametajwa kuwa ni msanii mashuhuri sana kwenye kutumia beef na kuanzisha uchokozi ili kutengeneza njia rahisi ya kuuzia kazi zake ambapo katika beef la mwaka huu Fity ameingia kwenye trends ya beef na mcheza ngumi maarufu wa uzito wa juu Floyd Mayweather ambaye alidai kuwa 50 Cent hana nafasi
tena kwenye muziki wa rap na  pia hana album
inayofanya vizuri sokoni ambapo kilicho fuata kama jibu kutoka kwa 50 Cent aliamua kuanzisha kampuni ya kusimamia mapambano
ya ngumi huku akimuandama Floyd Mayweather kuwa hajui kusoma na kuamua kumdharitisha kwa njia ya katuni na video pia.

Kadharika kuna hii pia kati ya Meek Mill na Wale ambapo Meeky alidai kuwa richa ya kuwepo katika Record Lebel moja na Wale alilalamika kuwa kitendo chake cha kutomsaport wakati anatangaza albamu yake "Dream worth than Money" ilionyesha dhahiri kuwa hampendi na yeye mwenyewe kuamua kumchukia.

Beef nyingine iliyo vuma sana ni kati ya Drake na Chris brown, kufuatia madai ya Drake kutoka kimahusiano na aliyekuwa mpenzi wa Chris Brown, Rihanna mwaka 2012 na kudaiwa kulianzisha tena kwa madai ya kuwa huenda akawa anatoka na mpenzi wake Chris wa sasa mwanadada   Karrueche Tran na kudaiwa kuwa ndio chanzo cha utengano wao.

Beef nyingine ya mwaka iliyo make headlines ni kati ya Tyga na Drake iliyosababishwa  na
Tyga kudai kuwa Drake ni mnafiki na si mtu halisia na kudai kutokana na hayo hampendi kabisa.

Nyingine ni hii hapa ambayo inakuwa beef ya tatu inayo muhusu Drake  kuharibu mahusiano ya watu kwa kuplay part ya u 'Play-Boy' ambapo katika hii ni juu yake na mwanamuziki  Common wote wakidaiwa kugombana kisa gwiji wa mchezo wa Tennis ‘ Serena Williams’.

Pia Kitendo cha Meek Mill kudai anaweza kurap hata kumzidi Cassidy king of rap kilimuuma sana Cassidy na kumfanya amchukie Meek Mill ambaye kwa upande wake alimuona kama bado kinda kwenye game ya Rap, richa ya Meek Mill kuambiwa
kuwa hawezi kushindana  na Cassidy na atapoteza heshima yake bure hasa akishindwa

Pia fahamu kuwa Manager wa Justin Bieber ‘Scooter’ alishawahi kuingia katika beef na Lil-Wayne baada ya kumkataza Bieber asijenge ukaribu sana na  mmoja wa ma rapper kutoka kundi la Young
Money ‘Lil Twist’ kwa madai kuwa ana tabia mbaya na nidhamu yake sio nzuri.

Ya mwisho ni hii hapa ya Jay Z kuwa na beef na ‘Cam'ron' huku chanzo kikidaiwa kuwa ni kufuatia kutangaza kuwa
makamu wa rais wa lebo ya Roc-A-Fella records
atakuwa Cam’ron ambaye ni rafiki wa Jim Jones na baadae kumtosa kufuatia madai ya aliyemteua, Dame Dash akiwa kama mmiliki wa
Record lebel hio akisaidiana na Jay Z kuamua kuuza hisa zake na Jay Z kuwa mmiliki halali bila ya kutimiza ahadi ni deni yakumpa Cam’ron na kuamua kumuacha kwenye mataa.

KWA MTAZAMO WAKO WEWE NANI NI MCHOKOZI ZAIDI KATIKA MOJA YA KILA BEEF HIZI?!!

ZIJUE 'BEEF' NANE ZA KIJINGA ZILIZO DUMU KWA MIAKA KADHAA HUKU ASILIMIA KUBWA ZIKIWAA ZA 2014 ZA WASANII WA HIP-HOP ZIJUE 'BEEF' NANE ZA KIJINGA ZILIZO DUMU KWA MIAKA KADHAA HUKU ASILIMIA KUBWA ZIKIWAA ZA 2014 ZA WASANII WA HIP-HOP Reviewed by Unknown on 13:20 Rating: 5

2 comments:

Powered by Blogger.