Recent Posts

UJASILIAMALI RAHA: JOKATE MWEGELO ASAINI MKATABA WA BILLIONI 8.5 NA KAMPUNI YA RAINBOW SHELL CRAFT KUTOKA CHINA.

Siku zote Mipango, Malengo, Uvumilivu na nafasi ya Mungu katika jambo fulani vikiungana lazima maendeleo yatazaliwa na huenda katika mbinu hiyo hiyo ndiyo aliyotumia mwanadada Jokate Mwegelo ambaye katika upande mwingine ni Mtangazaji wa runinga kupitia Tv1 ambapo ijumaa ya wiki iliyopita alifanikiwa kusaini mkataba kwa ajili ya Brand yake ya urembo ya  Kidoti aliyoianzisha yeye mwenyewe na kufanikiwa kuingia
mkataba na kampuni ya Rainbow Shell Craft ya
nchini China.

Jokate wakati akiongea na Waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa ilipo fanyika tafrija fupi ya Ubia huo alisema kuwa mkataba huo una gharama ya shilingi bilioni 8.5. Na kwamba malengo ya mkataba huo ni kujenga viwanda,
kufungua maduka na Kuiweka kampuni yake ya Kidoti kuwa brand
namba moja nchini na sehemu zinginezo.

Jokate alisema kuwa wamewekeza kiasi hicho cha fedha ili kuwezesha jambo hilo na mipango mingine zaidi katika shughuli za urembo.

"Ni kitu cha kunutunufaisha sote kwani ubia huu unalenga kuiwezesha Kidoti kuweza
kupanua wigo wake kibiashara ikitazama kujiweka
zaidi katika soko la Afrika Mashariki na kati na
kuendelea kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi,”
alisema Jokate.

Fahamu kampuni hiyo ya KIDOTI  inamiliki viwanda vya nywele na
bidhaa zingine za urembo ambapo pia Jokate alidai kunampango wa kutoa fursa kubwa ya ajira kwa Watanzania kupitia kampuni hiyo ikiambatana na bidhaa hizo kubuniwa na
wabunifu wa Kitanzania wa kampuni hiyo na
Rainbow ikitengeneza kile kilichobuniwa na kwamba
tayari zinapatikana kwenye supermarkert za
Uchumi.

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya  Rainbow
Shell Craft, Mr. Deng alisema kuwa katika kipindi
kifupi kampuni ya Kidoti itakuwa brand kubwa Afrika
Mashariki kutokana na mipango waliyo nayo kwa ajili yake.

“Kampuni ya Kidoti imeingia ubia na Rainbow hapa
Tanzania ili iweze kuwa bidhaa bora na
kuyependeza zaidi, Mpango ni kuzifanya bidhaa zianze kupatikana kwenye soko la Kariakoo ambako tunaamini itakuwa rahisi
kwa wananchi wengi kuzipata". alisema Jokate.

UJASILIAMALI RAHA: JOKATE MWEGELO ASAINI MKATABA WA BILLIONI 8.5 NA KAMPUNI YA RAINBOW SHELL CRAFT KUTOKA CHINA. UJASILIAMALI RAHA: JOKATE MWEGELO ASAINI MKATABA WA BILLIONI 8.5 NA KAMPUNI YA RAINBOW SHELL CRAFT KUTOKA CHINA. Reviewed by Unknown on 06:52 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.