Recent Posts

NEWS: ABIRIA 57 WANUSURIKA KUFA NA MMOJA KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI LA OSAKA.

ABIRIA 57 WANUSURIKA KUFA NA MMOJA KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI LA OSAKA.

Abiria 57 wanusurika kifo na mmoja kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyo husisha basi la Osaka lililokuwa likitokea Bukoba kwenda Dar - es salaam, baada ya basi hilo kugonga tela la lori lililokuwa limeegeshwa barabarani kutokana na ubovu na kutumbukia mtaroni.

Ajali hiyo ilitokea katika barabara kuu Dodoma/ Morogoro eneo la chuo cha biashara (CBE) kata ya
makole manispaa ya Dodoma majira ya saa sita usiku.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa ajali hiyo wameeleza kuwa dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T 197 BUS Scania,lililogonga tela la lori lenye namba za usajili T 533 BNM, lililokuwa likiendeshwa na Iddi Juma mwenye umri (41) liliharibika kabla halijatumbukia mtaroni na kujeruhi abiria mmoja.

Kamanda wa polisi mkoani Dodoma David Msime alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alisema kuwa
basi hilo la Osaka baada ya kushusha abiria stendi kuu ya mabasi, gari hilo liliondoka likiwa katika mwendo kasi na kushindwa kusimama pamoja na kusimamishwa na askari wa usalama barabarani waliokuwa kwenye eneo ambalo lori liliharibika na kuligonga.

Kamanda huyo aliongeza kuwa hakuna hata abiria mmoja aliypoteza maisha bali kulipatikana majeruhi mmoja aliyejeruhiwa vibaya katika ajali hiyo iliyotokea mkoani humo.

NEWS: ABIRIA 57 WANUSURIKA KUFA NA MMOJA KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI LA OSAKA. NEWS: ABIRIA 57 WANUSURIKA KUFA NA MMOJA KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA BASI LA OSAKA. Reviewed by Unknown on 10:35 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.