RAIS KIKWETE AWAPA MBINU POLISI.
Rais Jakaya Kikwete amelitaka jeshi la polisi Nchini kujiandaa kikamilifu ili kukabiliana na vurugu zozote zitakazojitokeza wakati wa uandikishaji wa wapiga kura, hasa kura ya maoni ya kupitisha katiba inayo pendekezwa na uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.
Raisi Jakaya Kikwete aliyasema hayo hapo jana wakati wa kufunga mafunzo ya maofisa waratibu,
na wasaidizi katika chuo cha Taaluma ya polisi jijiini Dar es salaam.
Sambamba na hayo rais Kikwete alisema kwamba dalili zinaonyesha kuwa kuna watu wenye nia ya
kuhatarisha amani katika matukio hayo hasa kwa jinsi yalivyo karibu kutokea.
Aidha rais Kikwete aliongeza kuwa serikali itahakikisha kazi ya uandikishaji katika daftari la
wapiga kura na upigaji wa kura ya maoni na uchaguzi mkuu vina fanyika kwa kulinda amani na
utulivu wa nchi yetu ya Tanzania.
Hata hivyo ameeleza kuwa vitatolewa vifaa mbalimbali ili kuhakikisha polisi wanafanya vizuri
na ulinzi mkali kutawala sehemu zote na kuondoa vurugu zote ,pamoja na kutunza amani kwa
umakini zaidi.
Iwapo mambo yote yatakwenda kama ilivyopangwa rais Kikwete amesema kuwa kura ya maoni ya
katiba inayopendekezwa itapigwa Aprili 30 - 2015 wakati uchaguzi mkuu utafanyika oktoba mwaka
huu.
No comments: