BRAZIL YAICHAPA UFARANSA 3-1.
>>Timu ya Taifa ya Brazili juzi imefanikiwa kuichapa timu ya Ufaransa mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa hapo jana.
Ufaransa ndio walikuwa wakwanza kuona lango la Brazil katika dakika ya 21 kwa goli lililofungwa na
Raphael Varane kwani ni kama waliichokoza kundi la nyuki kwani goli hilo lilirudishwa na Oscar dos
Santos Emboaba Júnior katika dakika ya 40, na hatimaye kushindiliwa magoli mengine mawili
kupitia kwa Neymar da Silva Santos, Júnior, na Luiz Gustavo na hivyo hadi mechi hiyo inamalizika
Brazil 3 Ufaransa 1.
Katika mechi nyingine za kimataifa za kirafiki zilizochezwa hapo jana, Bahrain iligeuzuwa chapati
na Colombia pale waliposhindiliwa magoli 6 kwa mtungi huku Iran ikiwapa darasa Chile kwa kuichabanga magoli mawili kwa nunge.
Jana pia kulikuwa na mechi moja ya kimataifa ya kirafiki ambapo Canada watairibisha Guatemala.
No comments: