WAANDISHI NA WANAHARAKATI WATIWA MBARONI NCHINI DRC.
Waandishi wa habari wa kigeni, wanadiplomasia na
wanaharakati pamoja na wasanii mbalimbali wametiwa mbaroni na polisi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakiwemo waandishi wa habari wa BBC.
Wanaharakati hao ambao ni vijana kutoka Nchini Burkinafaso senegal na kongo walikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuhusu jukwaa
jipya la kijamii.
Katika tukio hilo mwandishi wa BBC Maud Jullien aliripoti kuwa wanaharakati kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo,Senegal,na Burkinafaso walikuwa na mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Kinshasa
unaohusu kuundwa kwa jukwaa jipya la kijamii.
Waandishi hao miungoni mwa waliokamatwa walisema waliwaona polisi wakiwapiga baadhi ya
wanaharakati kwa kutumia marungu.
Lambert Mende ambae ni msemaji wa serikali ya Kongo alisema mkutano huo haukuwa halali na
kusema kuwa raia waliokamatwa kutoka Senegal na Burkinafaso ni wachochezi kwa usalama wa taifa la Kongo.
Raisi Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo atakamilisha muhula wake wa mwisho ifikapo Januari 2016.
Hata hivyo katika vurugu hizo watu takribani 40 waliuawa kutokana na kusababishwa na muswada wa uchaguzi ambao ungemuongezea muda wa kukaa madarakani Lambert Membe.
No comments: