Recent Posts

NEWS: HOSTEL YA MABIBO (MABIBO HOSTEL) JIJINI DAR-ES-SALAAM YAWAKA MOTO KUFUATIA HITILAFU YA UMEME.

HOSTEL YA MABIBO (MABIBO HOSTEL) JIJINI DAR-ES-SALAAM YAWAKA MOTO KUFUATIA HITILAFU
YA UMEME.

Moja ya Hostel wanayo ishi wanafunzi wa vyuo mbalimbali wakiwemo wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam imeungua moto kutokana na shoti ya umeme.

Tukio hilo la kuungua kwa hostel hiyo limetokea leo, majira ya saa tano na nusu (5:30) eneo la
mabibo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya mashuhuda na wanafunzi wanaoishi katika hostel hiyo, walisema kuwa tukio hilo lilitokea baada ya umeme kuleta shoti na
kupelekea kuungua kwa jengo hilo.

Hata hivyo baadhi ya wanafunzi walionekana kuwa na hasira kutokana na zimamoto kuchelewa kufika katika eneo la tukio na kusema kwamba foleni iliwachelewesha.

Zimamoto hao walipofika eneo hilo walipigwa na chupa na wanafunzi kutokana na kukuta tayari
wananchi wa eneo hilo wakishirikiana na wanafunzi
walishauzima moto huo.

NEWS: HOSTEL YA MABIBO (MABIBO HOSTEL) JIJINI DAR-ES-SALAAM YAWAKA MOTO KUFUATIA HITILAFU YA UMEME. NEWS: HOSTEL YA MABIBO (MABIBO HOSTEL) JIJINI DAR-ES-SALAAM YAWAKA MOTO KUFUATIA HITILAFU
YA UMEME. Reviewed by Unknown on 07:43 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.