MADRID, PORTO ZATINGA ROBO FAINAL UEFA, RONALDO AKIVUNYA REKODI.
>>Pamoja na Real Madrid kufungwa hapo jana naSchalke 04 ya Ujerumani kwa magoli 4 - 3 katika
mechi ya klabu barani ulaya timu hiyo imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano hiyo.
Real Madrid imenufanika na matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza ambapo iliwalaza Schalke 04 kwa jumla ya magoli 2- 0 na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla ya magoli 5 - 4.
Hapo jana Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo alivunja rekodi kuwa mchezaji pekee
aliyefunga magoli mengi katika michuano hiyo.
Ronaldo alifunga magoli 2 kati ya matatu ya Real Madrid na kufikisha jumla ya magoli sabini nane na
hivyo kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ya Real Madrid,
Raul.
Mchezaji anayemfuatia kwa karibu kwa kufunga mengi katika michuano hiyo kwa sasa ni Lionel
Messi ambaye hadi sasa ana magoli sabini na tano kwenye michuano hiyo.
Na katika mechi nyingine iliyopigwa hapo jana FC Porto ya Ureno nayo imeingia hatua ya robo fainali
ya michuano hiyo baada ya kuibamiza timu ya FC Basel ya uswis kwa magoli manne kwa mtungi.
Katika mechi ya awali timu hizo zilitoka sare ya goli moja kwa moja na hivyo FC Porto kuingia robo
fainali kwa jumla ya magoli Na leo kutakuwa na mechi nyingine za michuano hiyo ambapo Chelsea wanakaribisha Paris St Germain ya Ufaransa katika uwanja wa Stamford Bridge huku huku Bayern Munich wakipepetana na
Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
No comments: