MECHI ILIYOVUNJA REKODI YA KUCHEZWA KWA
MUDA MREFU.
>>Mechi ya Mchezo wa tenis kati ya raia wa Argentina Leonardo Mayer na Joao Souza wa Brazili
imevunja rekodi ya mchezo huo hapo jana kwa kuwa mechi pekee ya mchezo wa tenis kuchezwa
kwa muda mrefu kuliko wowote uliowahi kuchezwa katika michuano ya Davis Cup.
Katika mechi hiyo wachezaji hao walivunja rekodi iliyowahi kuwekwa mwaka 1982 katika michuano
hiyo baada kutumia saa sita na dakika arobaini na mbili ambayo ni zaidi ya dakika 20 ya ile iliyovunjwa
mwaka 1982.
Katika mechi hiyo Mayer wa Argentina alimfunga Joao Souza wa Brazil kwa jumla ya seti tano.
SPORTS: MECHI ILIYOVUNJA REKODI YA KUCHEZWA KWA
MUDA MREFU.
Reviewed by Unknown
on
08:12
Rating:
No comments: