NETANYAHU USO KWA USO NA OBAMA.
Waziri mkuu wa Israeli Benjamini Netanyahu, amewasili nchini marekani kupinga uwezekano wa
kufikia makubaliano na Iran juu ya mpango wake wa nyuklia.
Netanyahu amesema kuwa mkataba huo hautoshi kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.
Katika hatua hiyo Netanyahu anatarajiwa kulihutubia bunge la Congress jumanne ya kesho hotuba
ambayo haikukubaliwa kabla na utawala wa Raisi Barack Obama na kuiudhi Ikulu ya marekani.
Hotuba hiyo imeibuliwa wiki mbili kabla ya uchaguzi wa Israel huku chama chake cha Likud kikiwa katika shinikizo kwa ajili ya uchaguzi wa nyumbani.
Marekani na mataifa mengine yanayotambulikabkama p5+1 wanajadiliana na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.
Wanataka mpango wa makubaliano kufikia mwishoni mwa mwezi huu ambao unaeleza wasiwasi kuwa Iran inatafuta teknolojia ya silaha za
nyuklia jambo ambalo linakanushwa na Iran.
Aidha Barack Obama amesema hana mpango wa kukutana na Bwana Netanyahu, ikiwemo wafuasi kadhaa wa Demokratiki pamoja na makamu wa raisi huyo Joe Biden na hatahudhuria hotuba hiyo.
No comments: