MAN CITY YAICHAPA WEST BROM 3-0.
>>Mshambuliaji wa Mancity Wilfried Bonny alifunga bao lake la kwanza na kuiweka kifua mbele Mancity baada Gareth McAuley kupewa kadi
nyekundu katika mchezo uliochezwa juzi.
Fernandinho na David Silva waliongeza mabao mengine mawili na kuisaidia City kupunguza idadi
ya pointi kati yake na viongozi wa ligi Chelsea kuwa tatu hadi pale kikosi hicho cha Jose Mourinho kitakapocheza mechi zake mbili.
Hatahivyo mechi hiyo iliangazia sana kutolewa kwa mchezaji McAuley baada ya sekunde 89
pekee,ikiwa ni uamuzi wa mapema sana kufanywa katika ligi ya Uingereza msimu huu,ilipobainika
kwamba refa Neil Swarbrick alitoa kadi nyekundi kwa mtu ambaye hakustahili.
SPORTS: MAN CITY YAICHAPA WEST BROM 3-0.
Reviewed by Unknown
on
00:59
Rating:
No comments: