MVUA YAJAZA MAJI BARABARANI MAGARI NA WATU WASHINDWA KUPITA.
Mvua iliyonyesha kuanzia jana mpaka leo asubuhi,imeanza kuleta madhara mbalimbali kwa
wakazi wa Jijini Dar es salaam baada ya barabara nyingi kujaa maji.
Hali ni kwamba baadhi ya barabara zilijaa maji kutokana na mvua hiyo na wakazi wengi kushindwa kufika
muda muafaka kazini kutokana na tatizo hilo lililo dhibiti miundombinu kwa njia ya barabara mjini Dar es salaam huku waenda kwa miguu na waendesha magari wengi kuchelewa katika shughuli zao kwa kuwa wanapita kwa tabu.
KAY-STALLION TZ ilipita maeneo ya kawe na kushuhudia watu wakishindwa kutoka majumbani mwao kutokana na mvua kujaza maji mpaka kwenye milango ya kutokea, na kuwa lazimuka kusubili mpaka maji hayo yakauke ndipo
wapate kutoka nje.
Sambamba na hayo serikali tayari imeshaagiza wale wote waishio mabondeni waanze kuhama
kabla mvua hizi za masika hazija changanya kufuatia mabadiliko ya tabia ya Nchi ili kunusuru maisha
na mali zao.
No comments: