LUKAKU AIBEBA EVERTON EUROPA LEAGUE.
>>Mshambuliaji wa Everton, Romelu Lukaku jana aliisaidia timu yake ya Everton kupata ushindi dhidi
ya Dynamo Kiev ya Ukraine wa magoli 2 kwa moja.
Matokeo mengine ya mechi za mkondo wa kwanza wa ligi hiyo Villarreal ya Hispania ilishikishwa adabu na ndugu zao Sevilla baada ya kuchapwa jumla ya magoli 3-1.
Zenit Saint Petersburg ya Urusi wakaiadhibu Torino ya italia kwa magoli 2 kwa 0.
Nayo Fiorentina ya italia ikitoka sare ya goli moja kwa moja na AC Roma pia ya Italia.
Napoli ya Italia wakawapa kipigo cha mbwa mwizi Dynamo Moscow ya Urusi cha magoli 3 kwa moja.
Wolfsburg ya Ujerumani wakawa mwiba mkali kwa Inter Milan ya Italia pale ilipowashindilia magoli 3
kwa 1.
Mechi za mkondo wa pili wa ligi ya Europa zitaendelea siku ya Alhamis ya wiki ijayo March 19 mwaka huu.
No comments: