Recent Posts

NEWS: LONDON YAIFUNUA SANAMU YA GANDHI.

LONDON YAIFUNUA SANAMU YA GANDHI.

Sanamu ya shaba ya mgombea uhuru wa India, Mahatma Gandhi imefunuliwa rasmi mjini London
katika medani ya bunge la uingereza.

Mamia ya watu walihudhuria kutazama sherehe hiyo huku bendi ilipiga muziki wa kihindi na bendera za India zikipepea.

Kwenye sherehe hiyo waziri mkuu David Cameron, alimuelezea Gandhi kuwa kati ya watu mashuhuri
kabisa katika historia ya siasa duniani na alisema sanamu hiyo inampa makazi ya daima nchini
Uingereza.

Sanamu hiyo iko kando na sanamu za viongozi wa zamani kama Winston Churchill,ambae alipinga
harakati za Gandhi kuania uhuru kutoka uingereza.

Gandhi aliuliwa mwaka 1948 miezi michache baada ya india kupata uhuru wake.

NEWS: LONDON YAIFUNUA SANAMU YA GANDHI. NEWS: LONDON YAIFUNUA SANAMU YA GANDHI. Reviewed by Unknown on 10:16 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.