MASTAA WA TENNIS WAFUZU NUSU FAINAL.
>> Nyota wa tenesi Roger federer, Rafael Nadal na Novack Djockovic wametinga hatua ya robo fainali
ya michuano ya wazi ya BNP Paribas.
Federer alimchapa Jack Sock mwenye umri wa mika 22 kwa seti 6-3 6-2, kwa ushindi huo Federer atapepetana na Tomas Berdych wa Czech aliemfunga Lukas Rosol kwa seti 6-2 4-6 6-4.
Bigwa mara tatu wa michuano hiyo Rafael Nadal amefuzu hatua ya robo fainali baada ya kumchakaza Mfaransa Gilles Simon kwa seti 6-2
6-4,na atacheza na Milos Raonic, ambae alitinga hatua hiyo baada ya kumfunga Tommy Robredo wa
Ufaransa kwa seti 6-3 6-2, Novac Djokovic ambae ni bigwa mtetezi atachuana na Bernard Tomi,baada ya kumshinda John Isner
kwa 6-4 7-6. Huku Andy Murray akikabiliana na Feliciano Lopez raia wa Hispania, Murray alimshinda Adrian Mannarino katika mchezo wa
raundi ya mtoano.
No comments: