Recent Posts

NEWS: LOWASA: SIWEZI KUZUIA MAFURIKO KWA MKONO.

LOWASA: SIWEZI KUZUIA MAFURIKO KWA MKONO.

Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa monduli Edward Lowasa,alisema kuwa hawezi kuzuia wananchi kwenda nyumbani kwake kumshawishi agombee uraisi katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu na kudai ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mkono.

Lowassa alitoa kauli hiyo nyumbani kwake mjini Dodoma juzi wakati alipotembelewa na kundi jipya la Wananchi kutoka mbarali mkoani mbeya waliokwenda kumshawishi
atangaze nia ya kugombea uraisi.

Lowasa aliyahasa hayo siku moja baada ya katibu wa itikadi na uenezi wa Ccm Nape Nnauye kusema
kwamba kuandaa makundi ya kumshawishi mbunge huyo wa monduli anajua adhabu yake na
anaweza kupoteza sifa za kuwa mgombea uraisi kupitia ccm.

Lowasa alimalizia kusema kuwa utaratibu huo ulioanzishwa na watu, ni vigumu 'kuzuia mafuriko kwa mkono' ikiwa na maana kwamba hawezi kuwazuia watu kwenda kumtembelea.

NEWS: LOWASA: SIWEZI KUZUIA MAFURIKO KWA MKONO. NEWS: LOWASA: SIWEZI KUZUIA MAFURIKO KWA MKONO. Reviewed by Unknown on 03:14 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.