HALI BADO TETE UPATIKANAJI WA MIILI KATIKA AJALI YA NDEGE ILIYO TOKEA JANA.
Polisi nchini Ufaransa wame elezea kuwa hali ya hewa mbaya inayo endelea imezidi kukwamisha zoezi la utafutaji miili ya watu wapatao 150 katika eneo la
ajali yandege ya Germanwings A320 na hivyo huenda ikuchukuwa siku kadhaa kutafuta miili hiyo.
Siku ya jana ndege ya Ujerumani ya Germanwings A320 ilianguka katika eneo la milima ya "Alps" huko ufaransa na kuuwa watu wote wapatao 150 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Waathirika wa ajali hiyo walikuwa wanatoka nchi mbalimbali ambapo watu45 ni Wahispania huku zaidi ya 90 wakiwa ni Wajerumani.
Katika tukio hilo la kuhuzunisha na la kusikitisha la ajali hiyo watu 16, kati yao walikuwa ni wanafunzi kutoka shule moja nchini ujerumani ambao walikuwa wakirejea kutoka katika ziara ya
kutembelea nchi ya Hispania.
Pierre- Henry Brandet msemaji wa wizara ya mambo ya ndani iliwaambia waandishi wa habari kwa zoezi la kuuopoa na kutambua miili ndio kitu
kinachopewa kipaumbele.
Raisi wa Marekani Barack Obama amesema kwamba taifa lake linaungana na mataifa ya Ujerumani na Hispania katika kipindi hiki kigumu walichopoteza
wapendwa wao,na kwa sasa mawazo na sala nyingi kuelekeza kwa marafiki walioko ulaya na hasa watu wa nchi za Ujeruman na Hispania.
Obama aliongeza kuwa inaumiza kwa sababu ajali hiyo imepoteza watoto wengi kwa wakati mmoja na walio wengi ni watoto wachanga, na kudai kuwa
atawapigia simu viongozi wa nchi hizo mbili yaani Hispania na Ujerumani ili kuwapa salamu za rambirambi.
No comments: