Recent Posts

SPORTS: BIFU ZITO NDANI YA TOP 5 CHELSEA MAN CITY ARSENAL MAN U NA LIVERPOOL ZAGOMBANIA NAFASI.

BIFU ZITO NDANI YA TOP 5 CHELSEA MAN CITY ARSENAL MAN U NA LIVERPOOL ZAGOMBANIA
NAFASI.

>>Timu tano za juu katika msimamo wa Ligi nchini England zimeendelea kugombania nafasi za juu huku Man City, Arsenal, Man U na Liverpool zote kwa pamoja zikigombania kumaliza ama nafasi ya 2,3 na ya 4 ili kujikatia tiketi ya kushiriki Ligi ya
Mabingwa Balani Ulaya.

Katika michezo iliyopigwa hapo jana timu hizo zote tano zilifanikiwa kupata ushindi na kuendelea
kung’ang’ania katika nafasi zao.

Chelsea ambayo inapewa nafasi ya kuchukua ubingwa ilifanikiwa
kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya West Ham bao lililofungwa na Edin Hazard.

Man City wao walishinda kwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Leicester City mabao yaliyofungwa na David
Silva dakika ya 45′ na Milner dakika ya 88′ na kufikisha pointi 58 katika nafasi ya pili.

Nao Arsenal ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya QPR, kwa mabao ya Giroud 64′ Sánchez 69′ na kufikisha pointi 54 katika nafasi ya tatu.

Mashetani wekundu Manchester Utd wao walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle
bao lilifungwa na Wayne Rooney na kuifanya Utd kufikisha pointi 53 katika nafasi ya nne.

Kwa upande wa Majogoo ya Jiji Liverpool wao walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burnley
mabao yaliyofungwa na Henderson dakika ya 29 na ′ Sturridge 51′, Liverpool imeendelea kushika nafasi
ya tano ikiwa na pointi 51 huku ikizifuata kwa karibu Man U na Arsenal.

Matokeo mengine ya michezo iliyopigwa jana ni
kama ifuatavyo:-

Wed 4 Mar 2015 - Premier League
• Man City 2 - 0 Leicester
• Newcastle 0 - 1 Man Utd
• QPR 1 - 2 Arsenal
• Stoke 2 - 0 Everton
• Tottenham 3 - 2 Swansea
• West Ham 0 - 1 Chelsea
• Liverpool 2 - 0 Burnley
Tue 3 Mar 2015 - Premier League
• Aston Villa 2 - 1 West Brom
• Hull 1 - 1 Sunderland
• Southampton 1 - 0 Crystal Palace.

SPORTS: BIFU ZITO NDANI YA TOP 5 CHELSEA MAN CITY ARSENAL MAN U NA LIVERPOOL ZAGOMBANIA NAFASI. SPORTS: BIFU ZITO NDANI YA TOP 5 CHELSEA MAN CITY ARSENAL MAN U NA LIVERPOOL ZAGOMBANIA
NAFASI. Reviewed by Unknown on 14:45 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.