Recent Posts

NEWS: MCHUNGAJI GWAJIMA MIKONONI MWA POLISI KWA KUMTUKANA KARDINALI PENGO.

MCHUNGAJI GWAJIMA MIKONONI MWA POLISI KWA KUMTUKANA KARDINALI PENGO.

Mchungaji kiongozi wa kanisa la uzima na ufufuo lililopo kawe jijini Dar-es-salaam,Josephat
Gwajima amejisalimisha kituo cha polisi ilikuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Dar-es-salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Gwajima alimtukana na kumkashifu hadharani bila kujali taratibu na sheria za kidini na nchi kwa
ujumla.

Hata hivyo matusi hayo ni yale yaliyoonekana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii,ambapo
kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha mchungaji gwajima akimkashifu na
kumtukana kwa maneno makali Kardinali pengo katika hali ambayo iliwaudhi watu wengine.

Sambamba na hayo mapema jana asubuhi,kipande cha sauti ya Gwajima kilisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kilidai kuwa Gwajima ajisalimishe polisi siku ya jumatatu kwa kuwa
alikuwa Arusha na kuwataka waumini wake kufika polisi jumatatu bila vurugu za aina yeyote ile.

Mpaka sasa bado haijafahamika sababu zilizomfanya mchungaji huyo kujisalimisha siku ya jana, ijumaa badala ya jumatatu inayokuja.

NEWS: MCHUNGAJI GWAJIMA MIKONONI MWA POLISI KWA KUMTUKANA KARDINALI PENGO. NEWS: MCHUNGAJI GWAJIMA MIKONONI MWA POLISI KWA KUMTUKANA KARDINALI PENGO.
Reviewed by Unknown on 04:46 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.