PRINCE HERRY KUACHA JESHI MWEZI JUNI.
Mwanamfalme wa uingereza Prince Herry amesema kuwa anaangalia mustakhabali mwingine wa maisha baada ya kuthitisha kuwa ataacha jeshi mwezi wa juni.
Taarifa kutoka makazi ya kifalme ya Kensington ilisema Prince Herry atamaliza utumishi wake wa
miaka 10 jeshini baada ya wiki nne kwenda kutumikia katika jeshi la ulinzi la Australia kuanzia mwezi April.
Hata hivyo mrithi wa nne katika mfuatano wa warithi wa kiti cha mfalme wa uingereza walisema
uzoea wake jeshini utabakia katika maisha yake yote,lakini pia Prince Herry alisema bado alikuwa akitafakari ajira yake.
Prince Harry alishiriki mapigano mara mbili nchini Afghanistan, vita vya karibuni kabisa pale aliposhiriki mwaka 2012 akiwa rubani wa helkopta ya jeshini aina ya Apache.
Mwanamfalme huyo Prince Harry alitajwa kuwa rubani aliyetoa msaada mkubwa kwa wapiganaji wa ardhi kwa kuwajali.
No comments: