Recent Posts

NEWS: WALEMAVU WA NGOZI"ALBINO" WAZIDI KUTESEKA.

WALEMAVU WA NGOZI"ALBINO" WAZIDI KUTESEKA.

Matukio ya ukatili dhidi ya albino yameendelea kuwa tishio kubwa nchini Tanzania baada ya mtoto
wa miaka sita kukatwa kiganja cha mkono.

Shambulio hilo jipya kabisa limetokea mkoani Rukwa kusini Magharibi mwa Tanzania.

Mtoto huyo wa kiume Baraka Cosmas alikuwa amelala na mama yake mzazi wakati wahalifu hao
walipoivamia nyumba yao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Jackob Mwaruanda,alisema kwa sasa mtoto huyo anapata
matibabu katika hospitali na hali yake inaendelea vizuri,hata hivyo polisi bado wanafanya uchunguzi
kubaini wahusika wa tukio hilo.

Shambulio hilo limejitokeza baada ya wiki moja tu watuhumiwa wanne kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa
mauaji ya albino na muda mfupi baada ya rais Jakaya Mrisho kikwete kukemea mauaji ya albino ambao viungo vyao hutumika katika shughuli kishirikina kwa imani potofu kuwa zinasaidia kuleta utajiri na madaraka.

NEWS: WALEMAVU WA NGOZI"ALBINO" WAZIDI KUTESEKA. NEWS: WALEMAVU WA NGOZI"ALBINO" WAZIDI KUTESEKA. Reviewed by Unknown on 08:27 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.