CHAMBERLAIN NJE MWEZI MMOJA
>>Kocha wa Arsenal Arsene Wenger atalazimika kujikuna kichwa baada ya kupata habari kuwa kiungo chake cha kutegemewa Alex Oxlade-
Chamberlain hatakuwepo kwa takriban majuma tatu hadi nne zijazo kutokana na jeraha nyuma ya goti.
Kulingana na kochahuyo, Chamberlain alipata jeraha hilo katika mechi ya kukata na shoka ya FA dhidi yavwapinzani wao wa jadi Manchester United jumatatu
iliyopita.
Kujeruhiwa kwake ni pigo kwa azimio la Arsenal kuimarisha matokeo yao katika ligi kuu ya Uingereza ambapo sasa wanashikilia nafasi ya tatu.
Aidha Arsenal wanajiandaa kwa mechi ya marudio ya mkondo wa 16 bora katika ligi kuu ya mabingwa
barani Ulaya ambapo wameratibiwa kuchuana dhidivya Monaco juma lijalo.
Winga huyo alikuwa amerejea mwishoni mwa mwezi Februari baada ya kukaa mwezi mmoja nje kufuata jeraha lengine la kiuno.
Wenger hata hivyo alipata afueni katika safu ya ulinzi baada ya kurejea kwa Gabriel aliyejeruhiwa
katika mechi ngumu dhidi ya QPR mnamo Machi tarehe 4.
No comments: