Recent Posts

NEWS: AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MKOANI IRINGA YAUA WATU 42 NA KUJERUHI 22.

AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MKOANI IRINGA YAUA WATU 42 NA KUJERUHI 22.

Watu 42 wamefariki dunia papo hapo na wengine 22 kujeruhiwa baada ya ajali mbaya ya magari iliyo husisha basi la abiria na lori iliyotokea jana asubuhi
siku ya jumatano 11-3-2015 katika eneo la Changarawe Mufindi mkoani Iringa.


Ajali hiyo ilihusisha basi la abiria mali ya kampuni ya majinja Expres lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Dar es salaam ambapo liligongana uso kwa uso na
lori lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Iringa.


Kuhusu tukio hilo la kusikitisha mkuu wa polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alisema kuwa watu 42 walifariki dunia katika Ajali hiyo na wengine 22
kujeruhiwa ambapo baadhi ya majeruhi
walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi huku ajali hiyo ikihusisha gari la abiria lenye namba T438 CDE mali ya kampuni ya majinja, na idadi kamili ya watu waliofariki dunia kuwa ni wanaume
33, wanawake 6 na watoto 3.


Taarifa zaidi kutoka kwa watu walio kuwa katika eneo hilo la ajali wali sema kuwa maiti 32 bado hazijatambuliwa na ndugu ama jamaa.


Aidha Mungi wa polisi alielezea
kwamba chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kujaribu kukwepa moja ya shimo katika barabara,jambo lililosababisha lori hilo kutoka upande wake hadi upande wa basi abiria na kusababisha kugongana na basi hilo la kampuni
majinja Expres, ambapo baada ya kuvaana, na basi hilo kontena la futi 40 lililokuwa limepakiwa katika lori hilo liliruka juu na kwa kishindo kikubwa
kubamiza na kufunika basi hilo.


Mmoja wa majeruhi wa basi aliye jitambulisha kama Kevin Humphrey ambae amelazwa katika hospital ya
wilaya ya Mufindi alisema kuwa alisikia mshindo mkubwa baada ya basi hilo kugongana na lori hilo ambapo kontena lililotoka kwenye lori na kupiga juu
ya basi.

(MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.)

NEWS: AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MKOANI IRINGA YAUA WATU 42 NA KUJERUHI 22. NEWS: AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MKOANI IRINGA YAUA WATU 42 NA KUJERUHI 22. Reviewed by Unknown on 07:08 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.