Recent Posts

SPORTS: COUTINHO AIBEBA LIVERPOOL IKIIUA MAN CITY 2-1, ARSENA YAICHAPA EVERTON.

COUTINHO AIBEBA LIVERPOOL IKIIUA MAN CITY 2-1, ARSENA YAICHAPA EVERTON.

>>Phillipe Coutinho alifunga bao la ushindi na kuiwezesha Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuharibu matumaini ya Man city kulitetea taji lake katika uwanja wa Anfield.

Liverpool ilianza kupata bao kupitia kwa kiungo mwake Jordan Henderson katika dakika ya 11 na
kuiweka mbele Liverpool kabla ya Edwin Dzeko kusawazisha dakika ya 25.

Mnamo dakika ya 75 Mchezaji wa Brazil Philipp Coutinho alipachika bao la kuvutia alipofunga kutoka
nje ya eneo la hatari na kuifanya Liverpool kumaliza mchezo ikiwa na mabao 2-1.

Matokeo hayo yanaiweka Mancity pointi 5 nyuma ya Chelsea huku wakiwa wamecheza mechi moja zaidi nayo wakati Liverpool ikipanda hadi nafasi ya tano katika jedwali ikiwa na Point 48 na kujiongezea
matumaini ya kumaliza katika nafasi nne za juu.

Kwa upande wa Arsenal wao wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Evertoni huku mabao ya
Arsenal yakifungwa na Giroud dakika ya 39′ na Rosicky dakika ya 89.

Kwa ushindi huo Arsenal imepanda hadi nafasi ya tatu ikiwa na jumla ya pointi 51 ikiiacha Man U katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi.

SPORTS: COUTINHO AIBEBA LIVERPOOL IKIIUA MAN CITY 2-1, ARSENA YAICHAPA EVERTON. SPORTS: COUTINHO AIBEBA LIVERPOOL IKIIUA MAN CITY 2-1, ARSENA YAICHAPA EVERTON. Reviewed by Unknown on 01:18 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.