CHELSEA YABANWA NA SOUTHAMPTON YAAMBULIA SARE.
>>Chelsea imeendeleza uongozi wake katika ligi kuu ya Uingereza licha ya kutoka sare ya 1-1 dhidi
ya Southampton katika mechi ya msisimuko mkubwa iliochezwa katika uwanja wa darajani.
Diego Costa aliipatia Chelsea uongozi kupitia kichwa kizuri kabla ya Dusan Tasic kusawazisha
kupitia mkwaju wa penalti baada ya Nemanja Matic kumchezea visivyo Sadio Mane katika lango la Chelsea.
Kipa wa Southampton Frazer Forster alifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya Oscar,Eden Hazard na Loic Remy.
The blues sasa inaogoza ligi ikiwa na pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi wa ligi ya EPL Mancity
waliocharazwa bao moja kwa nunge dhidi ya Burnley.
SPORTS: CHELSEA YABANWA NA SOUTHAMPTON YAAMBULIA SARE
Reviewed by Unknown
on
07:22
Rating:
No comments: