MTANDAO WA KIISLAMU USO KWA USO NA "IS".
Viongozi wa kiislamu kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya wameanzisha jarida la mtandao katika juhudi za kukabiliana na itikadi kali za kidini zinazoendeshwa na wapiganaji wa islamic state.
Jarida hilo la kidigitali lenye jina la "Haqiqali" lenye maana ya "ama kweli" limezinduliwa na mtandao wa imani unaolenga kuwafunza vijana wadogo kuhusu ukweli wa makundi ya itikadi kali.
Wahusika wa Mtandao huo walisema kuwa wana wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa uvumi unaozushwa na makundi hayo katika mtandao ya kwamba jarida hilo jipya ndio njia pekee ya kukabiliana na uovu na mawazo mabaya wanayo itumia.
NEWS: MTANDAO WA KIISLAMU USO KWA USO NA "IS".
Reviewed by Unknown
on
04:34
Rating:
No comments: