WATU 7 WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE 48 KUJERUHIWA VIBAYA MKOANI MOROGORO KATIKA AJALI YA
GARI.
Ajali za barabarani zimeendelea kukatisha maisha ya Watanzania na kujeruhi wengi kutokana na
mwendo kasi wa magari.
Ajali hiyo ilitokea jana majira saa 6:45 mchana baada ya basi la msanga Line lenye namba za
usajili T.637 DCD linalofanya safari za Dar es salaam kwenda Mahenge wilayani Ulanga kugongana na basi la Luwinzo lenye namba T.453
AUA likitokea Njombe kwenda Dar es salaam.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Leonard Poul alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kudai
kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendosi kasi wa madereva wa mabasi hayo.
Hata hivyo kamanda huyo aliongeza kuwa majeruhi wa ajali hiyo wengi wao wapo katika Hospitali ya
St.Kizota iliyopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wakipatiwa matibabu.
No comments: