Recent Posts

NEWS: WAZIRI MKUU WA SINGAPORE AFARIKI DUNIA.

WAZIRI MKUU WA SINGAPORE AFARIKI DUNIA.

Waziri mkuu mwanzilishi wa Singapore Lee Kuan Yew amefariki dunia  akiwa umri wa miaka 91 kufuatia kuugua ugonjwa wa mapafu kwa muda mrefu.

Moja kati ya mambo ambayo waziri Lee Kuan Yew atakumbukwa nayo ni kufuatia kuleta mabadiliko
ya kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo walizokuwa nazo na kupelekea sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara.

Fahamu pia kuwa Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki
kati ya nchi yake na marekani ambao umedumu mpaka sasa.

Viongozi mbalimbali duniani kote wametuma salam za rambirambi kwa Singapore,baada ya kifo cha Lee Kuan Yew.

Lee Kuan Yew amefariki baada ya kuugua homa ya mapafu kwa muda
mrefu, ambapo Serikali ya Singapore imetangaza siku 6 za maombolezo hadi atakapozikwa siku ya juma pili wiki ijayo.

Hata hivyo Waziri wa Uingereza David Cameron alisema kuwa
Lee alikuwa mmojawapo wa viongozi wakuu duniani kutokana na mchango wake katika kuleta maendeleo.

NEWS: WAZIRI MKUU WA SINGAPORE AFARIKI DUNIA. NEWS: WAZIRI MKUU WA SINGAPORE AFARIKI DUNIA. Reviewed by Unknown on 04:32 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.