AL-SHABAAB WAUA WATU 10 SOMALIA.
Kundi la wapiganaji linaloshukiwa kuwa sehemu ya wanamgambo wa Al-shabaab, lilivamia hoteli moja
katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kufanya mauaji.
Taarifa toka Nchini Somalia zinasema kuwa Wanajeshi wa serikali ya Somalia wanaendelea kupambana na wanamgambo hao waliojihami kwa kulipua vipuli na bunduki za rasharasha,ambapo
katika tukio hilo watu 10 waliripotiwa kupoteza
maisha.
Kwa mujibu wa walioshuhudia wapiganaji hao wa Al-shabaab walisema kuwa walishambulia hoteli ya Makal-mukarama mjini mogadishu, ambayo ni hoteli maarufu mjini humo na inapendwa na watu wengi pamoja na wafanyakazi mbalimbali na mabalozi wa kimataifa.
Aidha balozi wa Somalia nchini Uswisi Yusuf Bari alinusurika kifo baada ya kukwepa kupigwa risasi na kupitia dirishani.
Kikosi maalumu cha kupambana na uvamizi wa aina hiyo kinaendelea kukabiliana na wapiganaji
hao ambao walisemekana kuwa walibanwa katika ghorofa ya juu ambapo sasa wanarusha mabomu ya kurusha kwa mkono (grenade) na
kufyatua risasi kwa yeyote anaye jionyesha mbele yao.
#Fahamu: Kundi la Al-shabaab limekuwa likitekeleza mashambulizi ya aina hii katika hoteli zinazosifika kuwa mahala pa burudani kwa wageni na viongozi mashuhuri serikalini.
No comments: