DAVID CAMERON ACHOKA KUENDELEA NA UONGOZI.
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kuwa hata weza kuendelea tena na wadhifa wake iwapo atarudi madarakani katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika siku zijazo mwezi mei 2015.
Cameron aliliambia shirika la utangazaji la "BBC" kuwa awamu ya tatu inaweza kuwa ni kipindi kirefu kwake kukaa madarakani hivyo inafaa awepo kiongozi mwengine mpya.
Hata hivyo chama kikuu cha upinzani cha "Leba" kilimshutumu waziri huyo kwa kuonyesha uzembe
na kushinikiza muhula wa tatu kwa chama chake cha "Conservative" hata kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi mkuu ujao.
NEWS: DAVID CAMERON ACHOKA KUENDELEA NA UONGOZI.
Reviewed by Unknown
on
06:35
Rating:
No comments: