Recent Posts

SPORTS: KLABU ZA ENGLAND ZAZIDI KUTESWA ULAYA.

KLABU ZA ENGLAND ZAZIDI KUTESWA ULAYA.

>>Jana usiku viwanja kadhaa viliwaka moto, katika michuano ya ligi ya Europa wakati timu kadhaa
ziliposhuka dimbani katika hatua ya 16 bora.

Everton ya England imetupwa nje ya mashindano hayo baada ya kuchapwa bao 5-2 dhidi ya Dynamo
Kyiv ya Ukraine, na kufanya matokeo ya jumla kuwa ni 6-4 baada ya mchezo wao wa awali
Everton kushinda nyumbani bao 2-1.

AS Roma imeangukia pua baada ya kuchabangwa mabao 3-0 nyumbani pale walipocheza na Fiorentina zote kutoka nchini Italy.

Kwa matokoe hayo Roma imetupwa nje kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wao awali.

Nayo Inter Milan ikakwaa kisiki baada kufungwa goli 1-2 dhidi ya Wolfsburg ya Ujeruman na
kuondoshwa pia katika mashindano hayo kwa magoli 5-2 baada ya awali kufungwa mabao 3-1,
huku Villarreal ikikaangwa goli 1-2 dhidi ya Sevilla na kubwagwa nje kwa goli 5-2 ambapo awali
walifungwa goli 3-1.

Mashindano hayo Europa kwa sasa yanaingia katika hatua ya robo fainali.

SPORTS: KLABU ZA ENGLAND ZAZIDI KUTESWA ULAYA. SPORTS: KLABU ZA ENGLAND ZAZIDI KUTESWA ULAYA. Reviewed by Unknown on 15:03 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.