Recent Posts

SPORTS: CHELSEA MABINGWA WAPYA CAPITAL ONE CUP.

CHELSEA MABINGWA WAPYA CAPITAL ONE CUP.

>>Klabu ya soka ya Chelsea imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa kombe la Capital one baada ya kuishushia kichapo cha mabao 2-0, timu ya Tottenham katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Wembley Jumapili jioni.

Katika mchezo huo Chelsea waliandika bao la kwanza katika dakika ya 45 ya mchezo huo kupitia
kwa nahodha wake John Terry, bao hilo lilidumu mpaka timu hizo zilipokwenda mapumziko.

Bao la pili lilipatikana dakika ya 56 baada ya mlinzi wa Tottenham Kyle Walker kujifunga katika harakati
za kuokoa hatari langoni kwake na kuwahakikishia vijana wa darajani ushindi wa kishindo .

Kombe hili ni la kwanza kwa kocha Mourinho tangu ajiunge kwa mara nyingine klabuni hapo mwaka
2013 akitokea nchini Hispania alikokuwa akiifundisha miamba ya soka nchini humo Real Madrid.

SPORTS: CHELSEA MABINGWA WAPYA CAPITAL ONE CUP. SPORTS: CHELSEA MABINGWA WAPYA CAPITAL ONE CUP. Reviewed by Unknown on 01:28 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.