Recent Posts

NEWS: POLISI WAADHIBIWA NA MEYA FERGUSON

POLISI WAADHIBIWA NA MEYA
FERGUSON.

Meya wa Mji wa Ferguson, jimboni Missouri James Knowles alitangaza hatua kadhaa wa kadhaa zitakazochukuli wa kufuatia ripoti iliyoonyesha ushahidi dhidi ya
polisi wa mjini humo kujihusisha na vitendo vya ubaguzi wa rangi.

James knowles alisema kuwa muajiriwa mmoja toka idara ya polisi alifukuzwa kazi na wengine
wawili walilazimishwa kwenda likizo baada ya kushutumiwa kutuma barua pepe yenye ujumbe wa
kibaguzi.

Knowles aliwaambia waandishi wa habari kuwa idara itaongeza namba ya maafisa wasio wazungu na kujikita katika mafunzo.

Meya alitoa kauli hiyo baada ya wizara ya sheria kufanya uchunguzi kuhusu kifo cha kijana mmoja
mweusi Michael Brown, aliyeuawa mjini humo na kubainika kuwa kulikuwa na viashiria vya ubaguzi wa rangi wakati tukio hilo.

NEWS: POLISI WAADHIBIWA NA MEYA FERGUSON NEWS: POLISI WAADHIBIWA NA MEYA FERGUSON Reviewed by Unknown on 08:19 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.