WENGER NA MATUMAINI YAKE UEFA.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa kilabu hiyo bado ina fursa ya kuibandua Monaco
katika michuano ya kilabu bingwa barani Ulaya licha ya kucharazwa 3-1 katika awamu ya kwanza
ya mechi hizo.
Arsenal itakabiliana na timu hiyo ya Ligi ya daraja la kwanza siku ya jumanne huku ikiwa hakuna
timu ilioweza kufanikiwa kubadilisha matokeo kama
hayo katika michuano hiyo.
Wenger:Tuna changamoto kubwa mbele yetu lakini tutafanya kila kitu kuhakikisha kwamba tunafuzu
kwa robo fainali.
''Wao ndio wanaopigiwa upato kufuzu lakini tunaweza kubadilisha mambo, Tutahakikisha kuwa tuna hamu na imani ya
kushinda''.
Arsenal italazimika kufunga bao tatu kwa bila ili kuweza kufuzu kwa robo fainali, Tayari kilabu hiyo imepata motisha kufuatia
ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya kilabu ya West Ham siku ya jumamosi. .
No comments: